Mabadiliko ya kwanza yaliyofanywa kwenye mechi ya nusu fainali katika michuano ya Olimpiki kwa wanaume kati ya Morocco dhidi ya Hispania yalikuwa ya mwamuzi.

Ilikuwaje? mwamuzi, Ilgiz Tantashev wa Uzbekistan, alionekana akichechemea katika dakika 15 baada ya kuangushwa kwa bahati mbaya na beki wa Hispania Marc Pubill aliyekuwa katika utekelezaji wa majukumu yake uwanjani.

Pubill alionekana kusukumwa na mchezaji wa Morocco alianguka na kwa bahati mbaya akajigonga kwenye mguu wa kulia wa Tantashev.

Mchezo huo ulisimamishwa kwa dakika chache wakati Tantashev akipokea matibabu.

Kwa bahati mbaya mwamuzi huyo ameshindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikachukuliwa na mwamuzi wa akiba Glenn Nyberg wa Uswis.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement