Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Azam Iddy Nado ameeleza furaha yake mara baada ya kuwa mmoja wa wachezaji wa Klabu hiyo kuipa mafanikio na kufanikiwa kufuzu kuiwakilisha Tanzania kunako michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Iddy Nado ameeleza kuwa alikuwa na ndoto ya kwenda kucheza michuano hiyo hivyo wanaamini kwa sasa ni wakati wa kupambana na kuonyesha kile walichonacho ili kufanya vizuri.

“Kwa mimi ninafuraha kwasababu ni mara yangu ya kwanza kwenda kushiriki michuano hii kwahiyo imekuwa furaha sana kwangu kwani ilikuwa ndoto yangu pia, ” Amesema Iddy Nado.

Kwa upande mwingine Nado ameeleza kuwa kila mchezaji anashahuku ya kwenda kushiriki katika michuano hiyo na anaamini viongozi wanapanga kuiandaa timu kwani mashindano hayo sio madogo hivyo kila mtu lazima aonyeshe ukubwa wake.

Nado kwa upande wake pia ameeleza kuwa wapo tayari kukutana na timu yoyote ya Afrika katika michuano hiyo kwani wanaamini maandalizi na jitihada vyote kwa pamoja vinaweza kuwapatia matokeo mazuri.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement