Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuhusu hali ya majeruhi katika timu hiyo kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali utakaochezwa Machi 30, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 3 usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamwe amesema kiungo Zawadi Mauya tayari ameanza mazoezi na yupo tayari kwa mchezo.

"Kibwana Shomari kwa mujibu wa daktari wa timu yupo katika asilimia 60 ya utimamu na bado hajaanza mazoezi.

"Pacome Zouzoua pamoja na Khalid Aucho wao wapo zaidi ya asilimia 80 ya utimamu wao na wameanza mazoezi.

Aliongeza: "Kwa upande wa Yao Kouassi bado ni asilimia 50/50 kwani bado hajawa timamu."

Yanga itacheza dhidi ya Mamelodi Sundowns mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ili kutafuta kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement