HUYU HAPA MUAMUZI WA MECHI YA SIMBA VS AL AHLY MISRI (PILATO)
Mwamuzi Jean Jacques Ndala kutoka DR Congo ameteuliwa kuchezesha mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya African Football League kati ya Al Ahly dhidi ya Simba SC utakaopigwa katika dimba la Cairo, Misri.
Ndala atasaidiwa na Jerson dos Santos wa Angola na Arsenio Marengula wa Msumbiji huku refa wa akiba akiwa ni Messie Nkounkou wa Congo.
Refa Ndala amekuwa na historia nzuri na Simba ambapo katika mechi tatu alizoichezesha, imeibuka na ushindi mara mbili na kupoteza mchezo mmoja ikiwa ni ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy, ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya RS Berkane na kipigo cha 2-0 dhidi ya JS Saoura.