Klabu zimetakiwa kuingia mikataba ya haki na sio ya utumwa na wachezaji wanaowasajili ili kuwa na maslahi ya pande zote mbili kwaajili ya kulinda haki za wachezaji.

Tumezungumza na Mwanasheria wa wachezaji ambaye pia ni Wakala wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni “FIFA” Hillary Ismail na kuweka wazi kuwa Klabu na wachezaji wanatakiwa kuwa na makubaliano kwaajili ya kuepusha migogoro na kuongeza kwa kuzitaka Klabu pia kutokumbana mchezaji kwa kuweka mashasti magumu kwa mchezaji anayetaka kuitumikia kabu nyingine iwapo yupo ndani ya mkataba.

Kwa upande mwingine Hillary amewataka pia wachezaji kuwa makini wanapotaka kusajili mikataba na Klabu kwa kuhakikisha wanazingatia kila kipengele katika mikataba hiyo kuielewa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement