HATUA YA MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA MAN U EUROPA INAWAITA
Matumaini ya Manchester United kufuzu kwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yametoka mikononi mwao inapoelekea katika raundi ya mwisho ya mechi za makundi.
Wenzao wa Ligi Kuu ya Uingereza Newcastle United pia wanategemea matokeo mengine yatakavyokwenda na timu zote za Uingereza lazima zishinde ili kuwa na nafasi ya kusonga mbele.
Wakati huohuo, mabingwa Manchester City na Arsenal tayari wamejikatia tiketi ya 16 bora kama washindi wa makundi.
Wataunganishwa katika hatua ya mtoano na RB Leipzig, Bayern Munich, Inter Milan, Real Madrid, Real Sociedad, Atletico Madrid, Lazio, Borussia Dortmund na Barcelona na PSV Eindhoven.
Matumaini ya Celtic ya Ulaya yalimalizika ikiwa imesalia mechi moja huku mabingwa hao wa Scotland wakipoteza kwa Lazio.
Timu mbili za juu katika kila kundi kati ya makundi manane zinafuzu katika hatua ya mtoano, huku nafasi ya tatu ikiingia kwenye Ligi ya Europa.
Manchester United lazima waifunge Bayern Munich Uwanja wa Old Trafford Disemba 12 na kutumaini Copenhagen na Galatasaray watoe sare mechi nyingine ili kutinga hatua ya 16 bora.
Iwapo United wataifunga Bayern na kuwe na mshindi katika mechi nyingine ya Kundi A, vijana wa Erik ten Hag watamaliza katika nafasi ya tatu na kushuka kwenye Ligi ya Europa.
Bayern Munich walitinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa wakiwa washindi wa kundi wakiwa wamebakiwa na mechi mbili baada ya kuifunga Galatasaray.
Copenhagen wataendelea na ushindi dhidi ya Galatasaray au wakitoka sare na United kushindwa kuifunga Bayern Munich.
Galatasaray lazima waipige Copenhagen ili kusonga mbele kwa sababu ya tofauti ya mabao na ukweli kwamba walitoka sare ya 2-2 katika mechi yao ya kwanza.