HATIMAYE LIGI YA TAIFA YA MPIRA WA KIKAPU IMEWEZA KUTOA MABINGWA WAPYA KUTOKA KWA WANAUME NA WANAWAKE
Ligi kubwa ya mpira wa kikapu Tanzania maarufu kama TAIFA CUP tumeshuhudia yakifikia tamati baada ya kurindima kwa takribani siku 11 tangu ilivyo anza Tarehe 19 pale makao makuu Dodoma viwanja vya Chinangali.
Kwa upande wa wanaume tumeshuhudia fainali kali Sanaa ambayo tumeona mkoa wa Kigoma wakiongozwa na Wachezaji bora kama Baraka Sadick, Mwalimu Heri, Ronaldo,Said Malowa n.k waliweza kuwafunga wenyeji Mkoa wa DODOMA kwa jumla ya points 58-54 na Kigoma kua bingwa mpya kwa mara ya kwanza
Kwa upande wa Wanawake tumeshuhudia timu ya Mkoa wa MARA ikiwa na Wachezaji kama Jesca Julius, Jesca LENGA, Witness Mapunda, TUMWAGILE n.k wameshinda kwa binde sana sana kwa alama 57-56 mbele ya Unguja, sasa hii imekua ni ubingwa wa kwanza kutoka kwa mkoa wa mara Katika ligi hii ya taifa cup.
Kingine kizuri katika mashindano haya upande wa Wanawake tumeshuhudia mbunge wa mkoa wa mara Ester Matiko nae alikua sehemu ya kikosi hicho kitu ambacho kinaongeza morali kwa vijana wengine.