HATIMAYE BINGWA WA UKANDA WA MAGHARIBI NA MASHARIKI WAFAHAMIKA NBA
Ni mara baada ya kutamatika mchezo wa 5 (Game 5) na kushuhudia mchezo mkali alfajiri ya leo timu ya Dallas Mavericks wameweza kushinda mchezo huu kwa points 124-103 na kupata bingwaa wa ukanda wa MAGHARIBI.
Kwa upande wa mashariki ni muda mrefu tulishuhudia bingwa ambae ni Boston Celtics ambae alimpiga fagio timu ya Indiana Pacers kwa kushinda Mechi zote nne.
Stori kubwa imekua ni Machezaji wa wawili ambao ni Luca Doncic na Kayrie Irving ambao wote kwa pamoja wamefunga points 72 yaani kila mmoja amefunga points 36.
Mbali na hiyoo Luca Doncic amechagiliwa kuwa MVP kwa ukanda wa MAGHARIBI kua mchezaji bora baada ya KUONESHA ubora mkubwa Sanaa na mchango mkubwa lakini kwa ukanda wa mashariki MVP alichaguliwa ni Jaylne Brown ambae ukanda ule alikua na kiwango boraa Sanaa.
Sasa swali kwa wapenzi wa Mpira wa kikapu ni nani atakua bingwa wa jumla je ubingwa utaenda magharibi au mashariki, kumbuka timu ya Boston Celtics inatafuta taji lake la 17 na kama itachukua ubingwa watampiku Lakers ambao nao wamebeba mara 17 Lakini kiujumla ukanda wa mashariki ndio wamebeba mara nyingi Zaidi 40 kwa 37 magharibi.