Serikali imesema viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2027 vinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2025 ambapo vitafanyiwa ukaguzi wa kikanuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Mei 20, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Mhe. Ussi Salum Pondeza aliyetaka kujua lini Serikali itawekeza kwa nguvu zote katika viwanja, walimu na mawakala wa michezo mbalimbali inayoonekana kuleta tija kwa Taifa.

Mhe Mwinjuma amefafanua kuwa Serikali inatekeleza ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu Arusha, Dodoma, Zanzibar (Fumba), Ilemela Jijini Mwanza pamoja na Akademia na Hosteli katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.

Pia ameongeza kuwa Serikali ipo katika ukarabati wa viwanja vya Benjamin Mkapa, Uhuru, Amaan na Gombani vya Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya CHAN 2024 na AFCON 2027, ukarabati wa miundombinu ya shule 56 za michezo pamoja na viwanja vitano (5) vya mpira wa miguu vya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ameeleza kuwa katika kuhakikisha uwepo wa walimu wa kutosha wa michezo, Mhe . Mwinjuma amesema Serikali imekuwa ikiongeza udahili katika vyuo vinavyotoa mafunzo ya walimu wa michezo hususani Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo hadi kufikia mwaka 2023/24 jumla ya wanafunzi 812 wamehitimu katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement