Hali ya majeruhi ya Liverpool imeongezeka huku Diogo Jota na Curtis Jones akiondolewa katika fainali ya  Kombe la Carabao wikendi hii dhidi ya Chelsea.

Uchunguzi umethibitisha kuwa wawili hao watakuwa nje ya uwanja na hawatapatikana kwa fainali ya Wembley, wakati Liverpool pia watakuwa bila Trent Alexander-Arnold.

Dominik Szoboszlai na Alisson pia wanatiliwa shaka sana kutokana na matatizo ya misuli ya paja.

Liverpool itasubiri kumfanyia vipimo zaidi kabla ya kuweka muda wa kupona lakini kuna wasiwasi kwamba Jota atakosekana hadi miezi miwili kutibia jeraha lake la goti.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement