Wakati mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ukifika tamati leo Desemba 10, 2023, timu zote 16 zina nafasi ya kufuzu robo fainali hali inayoashiria ugumu wa mashindano hayo msimu huu kulinganisha na matarajio ya wengi kabla hatua hiyo haijaanza.

Msimamo wa makundi manne ya mashindano hayo inaonyesha kuwa hata timu zinazoshika mkia hivi sasa zina nafasi ya kutinga robo fainali kulingana na namna zitakavyochanga vyema karata zao katika mechi tatu ambazo kila moja imebakiza na matokeo ya washindani wengine kwenye makundi yao.

Hali hiyo inatoa matumaini kwa Yanga na Simba zinazoivwakilisha Tanzania kwenye hatua hiyo kusonga mbele na kutinga hatua inayofuata licha ya kila moja kukusanya pointi mbili katika mechi tatu za mwanzo ilizocheza na kuzifanya zishike mkia.

Hadi wakati huu ambao hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefikia nusu ya mechi, hakuna timu iliyopoteza wala kushinda mechi zote tatu za mwanzo jambo lililopelekea kutokuwepo na utofauti mkubwa wa pointi baina ya kinara na timu nyingine. Kundi la maajabu zaidi ni A ambalo timu zote nne TP Mazembe, FC Nouadhibou, Mamelodi Sundowns na FC Pyramids zinalingana kwa pointi baada ya raundi tatu ambapo kila moja ina pointi nne ikishinda mechi moja, kutoka sare moja na kupoteza moja hali inayoashiria kuwa hata baada ya mechi ya raundi ya nne, hakutokuwa na timu itakayofuzu na pengine hilo litatokea katika raundi ya tano.

Katika kundi B, Asec Mimosas ina nafasi kubwa ya kutinga robo fainali kwani inaongoza ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Jwaneng Galaxy yenye pointi tatu, Wydad yenye pointi tatu na Simba iliyo na pointi mbili.

Vita kubwa katika kundi hilo inaonekana itakuwa kwa Simba na Wydad iwapo Asec itapata ushindi wa nyumbani katika mechi inayofuata dhidi ya Jwaneng na Simba inaweza kufuzu ikiwa itapata ushindi katika mechi ake tatu zilizosalia na hata kuongoza kundi iwapo Asec itateleza.

Kimahesabu, timu hiyo ya Ivory Coast inaweza kutofuzu au hata kushika mkia ikiwa itatafanya vibaya katika mechi zake zilizobakia.

Katika kundi C, utofauti wa pointi kati ya kinara na tỉmu inayoshika nafasi ya mwisho ni nne ambapo Petro Luanda inaongoza ikiwa na pointi saba ikifuativwa na Esperance yenye pointi nne wakati Etoile du Sahel na Al Hilal kila moja ina pointi tatu.

Licha ya kushika mkia katika kundi D na pointi mbili, Yanga ikipata ushindi katika mechi mbili zijazo dhidi ya Medeanma na CR Belouizdad inaweza kufuzu au kuongoza kundi kwani imezidiwa kwa pointi tano tu na Al Ahly inayoongoza msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Medeamna na Belouizdad ambazo kila moja ina pointi nne.

Ishara nyingine ya ugumu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ni vigogo watatu kati ya wanne wanaoongoza katika chati ya ubora wa klabu Afrika kutokuwa na uhakika wa kufuzu hadi sasa na hata wakishinda katika raundi ya nne.

Ishara nyingine ya ugumu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ni vigogo watatu kati ya wanne wanaoongoza katika chati ya ubora wa klabu Afrika kutokuwa na uhakika wa kufuzu hadi sasa na hata wakishinda katika raundi ya nne. Timu hizo ni Al Ahly, Mamelodi, Wydad na Esperance.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement