GUARDIOLA ASEMA ANAJUTIA KUTOMPA KALVIN PHILLIPS MUDA WA KUTOSHA MAN CITY
Kiungo huyo wa England (29), ambaye amefanya michezo miwili pekee ya kuanzia kwenye Premier League chini ya Guardiola, pia ameshindwa kuimarika wakati wa mikopo West Ham na Ipswich. Hajachezea City tangu Desemba 2023, na majeraha ya Achilles yalisababisha uhamisho wa majira ya joto kuvunjika.
Guardiola alipohojiwa kwa nini mambo hayajamwendea vizuri Etihad, alisema:
“Labda kwa sababu sikumpa dakika za kutosha. Wakati huo, Rodri alikuwa fiti na kama baba yetu, akiwalinda wana wengine 10. Pia mfumo wetu ulikuwa tofauti kabisa na Leeds. Wachezaji wanacheza vizuri wanapopewa mechi nyingi, na mimi sikumpa.”
Kocha huyo aliongeza kuwa Phillips ni “mtu mzuri sana” na sasa amerudi mazoezini na City:
“Tutajaribu kumsaidia, labda atacheza mechi kadhaa ili kupata tena kujiamini.”



