Klabu ya Singida Fountain Gate FC, imetolea ufafanuzi juu ya Mlinda Mlango wa Klabu hiyo, Beno Kakolanya hapo jana kutaka kupigana na watu wa Coastal Union FC katika Uwanja wa CCM Liti, ambao utatumika kwaajili ya mchezo wao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara hii leo.

Akizungumza hii leo, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate Fc, Hussein Masanza ameeleza kuwa, kilichotokea hapo jana ni hali ya mawasiliano ambayo hayakuwa sawa kwa pande zote mbili (Timu mbili) kwaajili ya kutumia uwanja huo kama sehemu ya mazoezi kuelekea mchezo wa hii leo.

“Jana palizuka hali ya sintofahamu katika Uwanja wetu wa amzoezi lakini pia katika Uwanja wetu wa amzoezi wa CCM Liti majira ya jioni, ambapo wenzetu, wageni wetu Coastal Union walikuwa na program ya kufanya mazoezi ya mwisho ya kujiandaa an mchezo kwahiyo ilitokea hali ya kuonekana kunaubishani,, ” Hussein Masanza

“Kilichotokea jana ni hali ya mawasiliano ambayo hayakuwa yamekaa vizuri kwa pande zote mbili, kwamaana ya Coastal Union walitakiwa kufika saa 10 jioni kwaajili ya kufanya maandalizi yao kama kanuni zinavyoelekeza, na tuliwapa ratiba hiyo, tuliwapa utaratibu huo, wakafika kweli saa 10, ”Hussein Masanza.

Masanza aliongeza kuwa, licha ya Coastal Union kuwahi kufika Uwanjani lakini walichelewa kuanza kufanya mazoezi kutokana na Meneja wa Uwanja kuchelewa kufika Uwanjani na kuchelewa pia kufanya mawasiliano na meneja wa Timu.

“Sisi kama Klabu na taratibu zetu zilivyo, tulitoka kambini na kuelekea Uwanjani kwaajili ya mazoezi, na tulifika saa 11 ambapo Coastal Union walitakiwa waondoke, lakini tukakuta ndio kwanza wao wanaanza, na ndio maana sasa kukawa na hali ya msuguano na baada ya pale tulizungumza na wenzetu na kujua kuwa ni hali ya mawasiliano tu,” Hussein Masanza.

Masanza ameeleza kuwa, kilichotokea ni hali ya kutokuelewana na ameshafanya mazungumzo binafsi na uongozi wa Coastal Union.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement