Golikipa wa Psg avamiwa nyumbani kwake
Mlinda mlango wa Paris Saint-Germain Gianluigi Donnarumma (24) na mke wake walikuwa wahanga wa uvamizi katika nyumba yao iliyopo Paris, usiku wa Jana Julai 20, 2023 ambapo walifungwa kamba, kupigwa na kuibiwa vito vya thamani vya takribani Euro laki 5.
Vyombo vya habari vinaelewa kuwa nyanda huyo raia wa Italia na mpenzi wake walifanikiwa kujihifadhi katika hoteli ya kifahari iliyo karibu saa 9:20 alfajiri ambapo walipatiwa msaada kabla ya wawili hao kupelekwa hospitali kupata huduma ya ziada.
Wafanyakazi wa hoteli hiyo waliwataarifu Polisi juu ya uvamizi huo huku uchunguzi juu ya wizi huo ukiangukia mikononi mwa kitengo cha Polisi wa Mahakama ya Paris cha Brigade de repression du banditisme.
Sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa PSG kuvamiwanl, itakumbukwa Angel Di Maria, Marquinhos, Sergio Rico, Mauro Icardi na Thiago Silva pia wamewahi kukumbwa na wizi wa namna hiyo.