Kipa wa Nigeria Stanley Nwabali, aliyetunukiwa nyota wa mechi.

Nwabali alianza soka kama mshambuliaji hadi makocha wake wa awali walipomgeuza kutoka mshambuliaji hadi kuwa kipa.

Nwabali anaiwakilisha klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini.

Nyota huyo amefungwa mabao mawili tu Afcon nzima, sare ya 1-1 dhidi ya Equatorial Guinea na sare ya 1-1, nusu fainali dhidi ya Afrika Kusini.

Amesema kuwa kipa wa ujerumani Manuel Neuer ndiye mfano wake na anavutiwa na ujuzi wa mdakaji huyo.

Mdakaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hakuamini kuwa angeanza mechi za Afcon za Super Eagles mbele ya kipa mwenza maarufu wa taifa Francis Uzoho.

Aliiwakilisha Nigeria kimataifa kwa mara ya kwanza mnamo 2021, Super Eagles ilipopata kichapo cha 4-0 kutoka Mexico, mechi ya kirafiki nchini Marekani.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement