Uongozi wa timu ya wanawake ya Geita Queens ya mkoani Geita iliyopanda kucheza ligi kuu ya wananwake Tanzania bara kwa msimu wa 2023-2024 pamoja na Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Geita wanawaomba wadau soka ndani na nje ya mkoa wa Geita ili kuisaidia timu hiyo kushiriki ligi kuu kutokana na timu hiyo kutokuwa na wadhamini.

Hayo yamebainishwa wakati wa Shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na Plan international chini ya mradi wao wa KAGIS wakikabidhi ahadi yao ya kutoa vifaa vya michezo na taulo za kike kwa timu hiyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4.

“Nitoe wito kwa wadau waendelee kutusapoti kadili wanavyojaliwa kuakikisha kwamba mahitaji yote ya msingi yanapatikana kambini lakini niwashukuru sana wadau maana kidogo tushindwe kufanya usajili lakini wadau wamejitokeza timu imesajili wachezaji wamelipwa stahiki zao na leo timu iko kambini ikifanya mazoezi kujiwinda na ligi kuu sio jambo dogo ni jambo kubwa sana. SALUM KULUNGE Mwekiti wa Chama cha soka mkoa wa Geita.

“Sisi tutachangia vitu vifuatavyo kulingana na maombi yaliyokuja,Tutachangia jezi pisi 30,tutachangia viatu pisi 30,tutachangia soksi pisi 30 pia,sheengurd pisi 30,mpira mmoja,Gloves pisi 4,net za magoli pea moja,lakini pia tutachangia sanitary pads pisi 60 reuserble na pisi 40 disposerble jumla pisi 100 kwaajili ya kambi, ELIUD MTALEMWA Meneja wa Mradi wa KAGIS

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Bi.Zahara Michuzi amewataka wachezaji wa timu hiyo kutokuiga tabia za kiume badala yake wabakie na mwonekano wa kike.

“Jamani mabinti zangu naomba basi tujiweke kidada akukufanyi wewe usiwe mchezaji mzuri mechi yetu ya kwanza ya ligi kuu sote tutaenda saloon tupendeze maana tukijiweka kama wakiume tutawapa wasiwasi wazazi wetu”ZAHARA MICHUZI Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita.

“Tunawashukuru kwa kitu kikubwa kama hichi mnaweza kukiona kama kidogo lakini ni kikubwa kwetu tunazidi kuwaomba zaidi watu wanaotaka kutusapoti waje watusogelee sisi tunapokea kitu chochote kile cha kuisaidia timu”JULIANA KIMARO Afisa Michezo Halmashauri ya mji wa Geita

“Kwanza tunawashukuru sana shirika la Kagis Kuja kututembelea katika kambi yetu na viongozi wetu kwa ujumla na tunazidi kuwakaribisha sana maana tuna mahitaji makubwa kwenye kambi yetu kama watoto wa kike na sisi kama wachezaji”JACKLINI FREDRICK Nahodha wa Geita Queens.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement