Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya mechi ya 'Kariakoo Derby' ataja mambo yanayoibeba timu hiyo na yaliyowapa ushindi jana Kariakoo Dabi.

Gamondi ameandika “Siri? Ni kupambana, kupambana na kupambana pamoja na kipaji, nidhamu na furaha yakuwa kwenye timu hii"

Yanga jana imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Simba katika Uwanja wa Mkapa yakifungwa na Kennedy Musonda kipindi cha kwanza, Maxi Nzengeli akifunga mawili kipinid cha pili, Aziz KI na msumari wa mwisho ulipigwa dakika ya 87 kupitia kwa Pacome Zouzoua aliyefunga kwa mkwaju wa penalt baada ya Che Malone kumfanyia madhambi Nzengeli katika eneo la hatari.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement