GAMONDI : HATUWEZI KURUDIA MAKOSA YALE YALE
Kikosi cha wachezaji 24 wa Yanga kimeondoka alfajiri ya leo kuwafuata Medeama SC, huku kocha mkuu Miguel Gamondi akiweka wazi kuwa dakika 180 za mechi mbili za kwaza zimempa mwanga sasa akili yote kwenye mchezo wa Ijumaa. Wakati mastaa hao 24 wa Yanga wakitajwa kusafiri alfajiri ya leo beki kisiki wa timu hiyo Joyce Lomalisa imethibitishwa kuwa yupo fiti tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Ijumaa saa nne usiku.
Gamondi alisema bado wana nafasi lakini pia anakazi kubwa ya kufanya yeye kama kocha kwa kuhakikisha anaiandaa timu ambayo itaweza kuendana na ubora na ugumu wa mashindano hayo hasa hatua ya makundi ambayo kila timu inahitaji kuongoza na kusonga mbele. "Pointi mbili tulizozipata tumezivujia jasho haikuwa rahisi hivyo zinahitajika mbinu zaidi kuelekea mchezo wetu na Medeama ili kujihakikishia nafasi ya kusonga;
"Makosa tuliyoyafanya hayawezi kujirudia tulikuwa bora dhidi ya CR Belouizdad tukapoteza kwa idadi kubwa ya mabao tukatulia na kusawazisha makosa kwenye mchezo uliofuata tumepata pointi moja baada ya sare mchezo unaofuata utakuwa mgumu lakini malengo ni pointi tatu." alisema. Gamondi alisema hakuna lisilowezekana kama watafanya maandalizi ya kutosha na kujiandaa vyema kuikabili Medeama huku akikiri kuwa amekaa na wachezaji wake kuwaeleza kuwa kila mchezo ulio mbele yao sasa ni fainali.
"Hatutakiwi kujiamini sana kama tulivyofanya makosa kwenye mechi mbili zilizopita naweza kukiri kuwa zimetupa darasa tunaingia kwenye mchezo wa ijumaa kwa kumuheshimu mpinzani; "Hatua hii ni ngumu na kila timu ina malengo yake ya kuvuka hatua inayofuata kundi letui licha ya kuwa wa mwisho bado tuna nafasi ya kuvuka tukiwekeza nguvu huko na kuweka heshima mbele bila kujali tunakutana na nani mechi mbili za mnwanzo zimetupa funzo hatutarudia makosa." alisema.
Wachezaji watatu wa timu hiyo wameachwa kwa sababu mbalimbali ambao ni Gift Fred, Crispin Ngushi na Denis Nkane. Nyota walioenda ni Dickson Job, Nickson Kibabage, Kouassi Yao, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, PacĂ´me Zouzoua, Jonas Mkude, Zawadi Mauya, Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli. Wengine ni Farid Mussa, Mahlatsi Makudubela, Moloko, Musonda, Mzize, Konkoni, Diarra, Metacha , Mshery, Bacca na Bakari Mwamnyeto.