GAMONDI AWAZUIA MASTAA WA YANGA KUGUSA MPIRA MAZOEZINI
KIKOSI cha kwanza Yanga sio poa. waulize winga Augustine Okrah na mshambuliaji Joseph Gueye wanacho pitia huko mazoezini.
Miguel Gamondi amewazuia kugusa kabisa mipira na kuwakabidhi kwa watu wawili. Guede ambaye ametua kambini hivi karibuni baada ya kuanza mazoezi hadi sasa jamaa hajagusa uwanja kwa kucheza na wenzake mazoezini,amendelea kuimarishwa kwa mazoezimakali nje ya uwanja.
Guede amekuwa akikimbia mbio tofauti nje ya uwanja akiwa chini ya kocha wa mazoezi ya viungo Taibi Lagrouni ambapo muda mfupi hupewa mapumziko ya kunyoosha viungo nakuchezea mpira kisha kuhamia kwa daktari wa viungo Youssef Ammar kuangaliwa kama kila kitu kwake kipo sawa.
Wakati Guede akihamia kwa Ammar, zamu inamgeukia Okrah ambaye naye bado hajaanza kucheza na wenzake tangu apone jeraha la usoni alilolipata kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Mapema kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisema kuwa Guede hataharakishwa kuingia kwenye mazoezi na wenzake mpaka watakapo muweka kwenye daraja sawa la ufiti sambamba na wachezaji wenzake na mazoezi hayo yanasaidia kuinua kiwango na kuwa sambamba na wenzake pamoja na kujifunza mambo kadhaa kwa wenzake.
"Ukichelewa lazima ratiba kama hii yamazoezi ambayo wenzako waliyapata utalazimika kuyapata ili muweze kuwa sawa kwa ubora, tunataka kumuimarisha zaidi awe tunapotaka,'alisema Gamondi ambaye timu yake ilicheza mechi ya FA jana usiku dhidi ya Hausung.
Ratiba ngumu zaidi ya wawili hao nipale wanapokuwa na Lagrouni ambaye mazoezi yake yamekuwa magumu kwa mastaa hao huku akiwa mkali anapoona kasi anayotaka inapungua ilhali Gamondi akiwa pembeni akishuhudia matizi ambayo hufanyika makusudi kabisa.
Gamondi na jopo lake wameamua kukomaa na usiriazi wa mazoezi kwa mastaa wake kwa maelezo kwamba ratiba iliyopo mbele yao ni ngumu, hivyo wasipokuwa makini wanaweza kujikuta wakipishana na malengo ya klabu hiyo.