Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Februari akimshinda Abdelhak Benchikha wa Simba na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons walioingia naye fainali.

Hii ni tuzo ya pili kwa kocha huyo baada ya kutwaa ya mwezi Agosti, mwaka jana ambayo alikabidhiwa muda mfupi kabla ya mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa ugenini wakishinda mabao 3-1.

Gamondi ameiongoza Yanga kwenye michezo mitano ikishinda minne na suluhu moja na kupanda kutoka nafasi ya pili hadi ile ya kwanza.

Kocha huyo ameiongoza timu hiyo dhidi ya Kagera Sugar ikitoka suluhu, akashinda dhidi ya Dodoma Jiji bao 1-0, Mashujaa 2-1, Tanzania Prisons 1-2 na KMC 0-3.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement