Yanga walikua wa kwanza Kupata Bao Kipindi cha Kwanza Dakika ya 8 Kupitia AZIZ Ki goli ambalo lilidumu mpaka dakika ya 18 ambapo Sillah alisawazisha na kuwapa goli Azam FC na dakika 45 kuisha zikiwa wametoshana Nguvu wote

Kipindi cha Pili kilianza na kasi sana na Azam wakapata Goli la kuongoza dakika ya 62 kupitia mkwaju wa penati lakini AZIZ Ki alirudi tena wavuni kwa mkwaju wa Adhabu nje ya 18 na kuweka 2-2 dakika 68

Aziz Ki aliandika Hat Trick yake siku ya leo na ya kwanza kwenye msimu huu akiipa goli la kuongoza YANGA Dakika ya 71 na kuifanya YANGA Kuwa 3-2 Uwanja wa Benjamin Mkapa 


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement