Shirikisho la Soka Uganda, FUFA, limezindua mpira rasmi utakaotumiwa katika mechi.

Umetengezwa na Janzi - mtengezaji rasmi wa mavazi, FUFA. Mpira huo utatumika kwenye mashindano yote ya FUFA yakiwemo Ligi Kuu ya Startimes Uganda, na mashindano mengine ya soka.

Mpira wenyewe umepewa jina la Zakayo ambalo ni jina la Sokwe maarufu nchini Uganda, na kuweka urithi hai wa Sokwe huyo.

Sokwe Zakayo, alifariki mnamo 2018 akiwa na umri wa miaka 55.

Alizaliwa katika Hifadhi ya Taifa ya Semiliki kabla ya kuhamishiwa hadi Hifahi ya Entebbe (Uganda Education Wildlife Centre).

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement