Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA) kimtoa onyo kwa shirikisho la soka duniani FIFA na kueleza kuwa wako tayari kugoma kutokana na kalenda ya mechi kuwaba.

Mtendaji mkuu wa PFA Maheta Molango amezungumza wakati chama cha wachezaji duniani FIFAPRO kinaongoza kesi ya pamoja na ligi kadhaa za Ulaya, ikiwa ni pamoja na LaLiga na Ligi Kuu.

Siku mbili kwamaana ya Mei 30 kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund jijini London, Ligi Kuu ya Uingereza, LaLiga, Serie A na PFA zilikutana ili kuchunguza hatua za kukabiliana na nia ya FIFA ya kuongeza idadi ya mechi ambazo wanasoka watalazimika kuvumilia msimu ujao.

Mkurugenzi Mtendaji wa PFA, Maheta Molango, ambaye amekuwa akitaka mabadiliko tangu Februari, anaamini kuwa wachezaji wamefikia pabaya na kuweka wazi kuwa ratiba nyingi za soka zinahatarisha afya za wachezaji na kupunguza ubora wa mchezo huo.

Muungano wa wachezaji wa kimataifa FIFPRO, pamoja na PFA na Shirikisho la Ligi za Dunia (WLA), wanaendelea kutishia hatua za kisheria ikiwa FIFA haitabadilisha mkondo.

Katika barua iliyotumwa kwa Rais wa FIFA Gianni Infantino na katibu mkuu Mattias Grafstrom, walielezea wasiwasi wao juu ya upanuzi wa michuano mipya ya Kombe la Dunia la Klabu yenye timu 32.

Kwa kujibu, FIFA ilikanusha madai yao kuwa imechukua maamuzi ya upande mmoja kupendelea mashindano yake katika kalenda ya kimataifa na haitafikiria kupanga tena mashindano.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement