FIFA yazifungia Kitayosce, Fountain Gate kusajili wachezaji wapya.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa taarifa ya kufungiwa kusajili wachezaji kwa klabu ya Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu msimu ujao na Fountain Gate inacheza Championship.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo ulikuja baada ya vilabu hivyo kwa nyakati tofauti kumvunjia mkataba Kocha Ahmed El Fafamawy Yousef Mostafa Soliman bila ya kufuata utaratibu.
"Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu FIFA baada ya kocha Ahmed El Fafamawy Yousef Mostafa Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya Klabu hizo Kocha huyo raia wa misri ambaye amezifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti alifungua kesi FIFA akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu." ilisema taarifa hiyo
"Baada ya Soliman kushinda kesi Klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya Siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini hazikutekeleza hukumu hizo"