FIFA IMEWATEUA WAAMUZI WANNE WA CECAFA KWAAJILI YA KWENDA KUCHEZASHA OLIMPIKI PARIS 2024
FIFA imewateua waamuzi wanne kutoka baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuchezesha michezo ya Olimpiki Paris nchini Ufaransa 2024.
Michezo ya Olimpiki ya Paris ya 2024 ambayo itashirikisha taaluma 32 za michezo ikiwemo kandanda itafanyika Julai 26 hadi Agosti 11 nchini Ufaransa.
Waamuzi waliochaguliwa kutoka CECAFA ni pamoja na; Ismail Mohmood Ali (Sudan), Ahmed Liban Abdoulrazack (Djibouti), Stephen Yiembe (Kenya) na mwamuzi wa kike Shamira Nabadda kutoka Uganda.
FIFA imeteua waamuzi 21, wasaidizi 42, wasimamizi 20 wa mechi za video na wasaidizi 6 ambao watakuwa wasimamizi wa kitengo cha wanaume na wanawake. Wasimamizi kumi wa mechi kutoka Afrika wameteuliwa na FIFA.