FEISAL SALUM (FEI TOTO) KUPIGWA FAINI YA SHILINGI 500,000.
Fei toto kutozwa Shilingi 500,000 na kufungiwa mechi tatu kila mmoja, linawanyemelea Mudathir Yahya wa Yanga na Feisal Salum 'Fei Toto' wa Azam kutokana na kosa la kutosalimiana na wachezaji wenzao katika mchezo baina ya timu zao uliochezwa juzi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Muda mfupi kabla ya mchezo huo kuanza, Feisal na Mudathir walifanya kosa hilo baada ya kutegeana kuingia uwanjani katika muda ambao wenzao walikuwa wanasalimiana.
Kwa mujibu wa kanuni kanuni ya 41:5 (5.4) kufanya kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa kiwanjani, kukataa kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa au kuonesha ishara inayoashiria matusi.
Fei Toto alikuwa anafanya mazoezi ya viungo kwa kunyoosha miguu huku Mudathir akikung'uta viatu vyake ikionekana ni ujanja wa kila mmoja kumtegea mwenzake aanze kuingia uwanjani kitendo ambacho kanuni za ligi zinakitafsiri kama kutokuwa na uungwana lakini pia kikihusishwa na imani za kishirikina. Mastaa hao walikuwa nje kwa muda wakati wachezaji wengine wakijipanga na kusalimiana, Feisal na Mudathir waliendelea kutegeana hadi zoezi hilo lilipokamilika huku kila kikosi kikienda upende wake. Wakati taharuki kwa mashabiki ikiwa kubwa baada ya kustukia kitendo hicho, ndipo Mudathir alipoamua kuwa wa kwanza kwenda kuungana na wenzake huku Feisal naye akifuata na kupiga picha za vikosi.
Msimu uliopita mastaa wa Simba na Yanga, Clatous Chama, Stephane Aziz Ki walilipishwa faini ya shillingi 500,000 na kufungiwa kuto kucheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara zilizokuwa zinafuata. Ilielezwa kwamba katika mechi namba 64 ambayo iliwakutanisha Yanga na Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 23, 2022, Chama na Aziz Ki walikwepa kusalimiana.