FARU WEUSI WA NGORONGORO KUIHESHIMISHA TANZANIA KIMATAIFA
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngumi ya Tanzania maarufu kama "Faru Weusi wa Ngorongoro" wamefanikiwa kuiheshimisha Tanzania katika michezo ya 13 ya Afrika kwa maana ya All African Games 2023 Jijini Accra nchini Ghana iliyofungwa rasmi usiku wa jana katika Jiji hilo.
Kikosi hicho kimefanikiwa kushinda Medali tatu za shaba katika mashindano hayo kutoka kwa wachezaji Yusuf Changalawe ambaye ni Nahodh wa kikosi hicho, Ezra Paulo na Musa Maregesi ambapo wachezaji wote hao wanatokea katika Klabu ya Ngome inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Kikosi hicho cha Faru Weusi wa Ngorongoro pamoja na wachezaji wa michezo mingine walioiwakilisha Timu Tanzania katika michezo hiyo, wanatarajia kurejea Dar es salaam kuendelea na mazoezi ya kujiandaa kushiriki mashindano ya Mandela Maarufu kama "Mandela Cup" yatakayofanyika Durban nchini Afrika ya Kusini kuanzia tarehe Aprili 15 mpaka 23 mwaka huu.
Mbali na mchezo wa ngumi Katika michuano ya All African Games Tanzania iliwakilishwa na washiriki 109 katiia michezo sita ambayo ilijumuisha wanamichezo na wataalamu katika michezo ya kriketi wanaume na wanawake, judo, baiskeli, kuogelea na mpira wa miguu wanawake chini ya Umri wa miaka 20.