FAINALI ZA NBA ZINAZIDI KUNOGA MARA BAADA YA BOSTON CELTICS KUZIDI KUMCHAKAZA DALLAS MAVERICKS
Alfajiri ya leo TIMU ya Boston Celtics chini ya kocha Jose Mazulla kimeendeleza ubabe mbele ya timu ya Dallas Mavericks baada ya kuinyuka kwa points 105-98 Katika mchezo wa pili(game 2)
Game ya 2 bado Kocha Jose Mazulla ameendelea kumzidi maarifa kocha Jason Kidd na maraa hii ameendelea kuonesha ubora namna ya kujilinda na kuzuia(offensive and defensive playing)
Katika mchezo huu mchezaji Luca Doncic amekua na takwimu bora baada ya kufunga points 32 lakini bado hajaisaidia timu yake kushinda mbali na Luca Doncic Wachezaji wenzake Washington,Jones Jr na Irving wamecheza vizuri lakini bado hawakufurukuta
Kwa upande wa Boston Celtics Wachezaji kama Holiday, Brown,Tatum, White walikua na kiwango bora sanaa lakini Holiday alifunga points nyingi zaidi kwa upande wa Celtics 26
Baada ya matokeo hayo ya points 105-98 Sasa Boston Celtics watasafiri mpaka AAC ARENA (American Airlines Center) kwajili ya game 3 na 4 kwajiri ya kuweza kurejesha matumaini kitu ambacho kwenye Mchezo wa kikapu kinawezekana
Mbali na hiyoo kocha wa Dallas Mavericks mr Jason Kidd kabla ya mchezo aliulizwa kuhusu Jalren Brown akasema ni mchezaji bora na anastahiri kua mchezaji bora katika FAINALI hizi