Shirikisho la soka barani Afrika limepanga fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kufanyika mwezi Desemba, 2025 hii ikiwa ni baada ya vuta nikuvute kuhusu muda wa fainali za Mataifa ya Afrika za 2025 zitakazofanyika nchini Morocco.

Nchi mwenyeji kupitia kwa Rais wake Fouzi Lekja ilikuwa imetangaza kuwa Mashindano hayo yatachezwa majira ya joto ya 2025.

Hata hivyo, kutokana na ratiba ya Kombe la Dunia la vilabu ambalo litafanyika majira ya joto na kusababisha kufanyika kwa wakati mmoja jambo hilo lilizua mijadala mingi miongoni mwa wadau wa mchezo huo.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Makao Makuu ya CAF mjini Cairo, Misri, michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili sasa imepangwa kufanyika Desemba 2025.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement