FAINALI CWC, VITA YA KUSAKA REKODI NA HESHIMA YA DUNIA
Chelseana PSG zinakutana kwenye Fainali ambayo wapenda soka wengi wanaamini kutakuwwa na idadi kubwa na mabao yasiyopungua manne kutokana na ubora wa kila timu sambamba na kuwa na safu nzuri za ushambuliaji.
Chelsea chini ya Kocha Enzo Maresca itapambana kufukuzia rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya England kubeba Ubingwa wa Dunia mara mbili baada ya kufanya hivyo mwaka 2021 ilipoichapa Palmeiras.
PSG kwa upande wao utakuwa ni ubingwa wa kwanza licha kwenye kikosi chao kutakuwa na watu watakaokuwa wameboresha zaidi rekodi zao za Ubingwa wa taji hilo akiwepo Kocha Luis Enrique.
Rekodi zinaonyesha Chelsea na PSG hazijawahi kukutana tangu mwaka 2016 wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa jumla Chelsea imewahi kushinda mara mbili dhidi ya PSG wakati wababe hao wanaonolewa na Luis Enrique yenyewe wameshinda mara tatu huku mechi Tatu zikimalizika kwa sare.



