Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Wes Brown amesema staa wa Al Nassr na Ureno ajiandae kwa majukumu tofauti na yale aliyozoea katika kikosi cha timu ya taifa kwenye mashindano ya Euro mwaka huu.

Ronaldo ambaye atakuwa nahodha wa Ureno kwenye kulisaka taji lao la kwanza la Euro tangu mwaka 2016, anaonekana atapunguziwa majukumu kutokana na umri wake.

Akizungumza na Thrash podcast, Wes Brown alisema: “Nafikiri atakuwa anaanza kikosi cha kwanza lakini sidhani kama atamaliza mchezo, najua ataelewa uamuzi huo, hawezi kuanzia benchi kwa sababu ni mchezaji mkubwa ambaye ana rekodi ya kipekee kwenye michuano hii na Ureno kwa jumla.

“Nafikiri hii ndio itakuwa njia rahisi kwake, pia sidhani kama atachezeshwa nafasi tofauti na ile aliyozoeleka kuichezea, naona atakuwa anaanza na kucheza kwa dakika kadhaa kisha atatoka.”

Fundi huyu anayemilikiwa na matajiri wa Saudia pia ndio mfungaji bora wa muda wote hadi sasa akiwa na mabao 14.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement