Jarida la Football Finance limeweka bayana mishahara ya makocha wote 24 walio na timu za huko kwenye Euro 2024. Na kwenye mkeka huo, kocha wa England, Gareth Southgate, ndiye anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwa waliopo Euro 2024, akilipwa mara 29 zaidi ya pesa anayochukua kila mwaka kocha Willy Sagnol, ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Georgia.

Makocha kama Roberto Martinez na Julian Nagelsmann wanahitaji kulipwa mishahara mikubwa kwa sababu wanafanya kazi ya kuzinoa timu kubwa kama za Ureno na Ujerumani.

Lakini, mishahara mikubwa wanayolipwa makocha hao inakwenda sambamba na presha zinazowakabili katika kuhakikisha mataifa yao yanafanya vizuri kwenye fainali hizo. Kinyume cha hilo, basi mwisho wa michuano hiyo ya Euro 2024 basi chochote kinaweza kutokea kwenye hatima za vibarua vyao.

ORODHA YA MISHAHARA YA MAKOCHA WA EURO 2024 WANAYOLIPWA KWA MWAKA

1. Gareth Southgate (England, Pauni 4.9 milioni), 2. Julian Nagelsmann (Ujerumani, Pauni 4 milioni), 3. Roberto Martinez (Ureno, Pauni 3.4 milioni), 4. Didier Deschamps (Ufaransa, Pauni 3.2 milioni), 5. Ronald Koeman (Uholanzi, Pauni 2.5 milioni), 6. Luciano Spalletti (Italia, Pauni 2.5 milioni), 7. Vicenzo Montella (Uturuki, Pauni 1.5 milioni), 8. Murat Yakin (Uswisi, Pauni 1.4 milioni), 9. Ralf Rangnick (Austria, Pauni 1.3 milioni), 10. Domenico Tedesco (Ubelgiji, Pauni 1.3 milioni), 11. Zlatko Dalic (Croatia, Pauni 1.3 milioni), 12. Dragan Stojkovic (Serbia, Pauni 1.2 milioni), 13. Luis de la Fuente (Hispania, Pauni 1 milioni), 14. Serhiy Rebrov (Ukraine, Pauni 1 milioni), 15. Kasper Hjulmand (Denmark, Pauni 970,000), 16. Sylvinho (Albania, Pauni 632,000), 17. Michal Probierz (Poland, Pauni 472,000), 18. Steve Clark (Scotland, Pauni 464,000), 19. Francesco Calzona (Slovakia, Pauni 455,000), 20. Marco Rossi (Hungary, Pauni 253,000), 21. Matjaz Kek (Slovenia, Pauni 253,000), 22. Ivan Hasek (Czech Republic, Pauni 210,000), 23. Edward Iordanescu (Romania, Pauni 202,000) 24. Willy Sagnol (Georgia, Pauni 168,000)

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement