Mwanasoka nyota wa zamani wa Cameroon na Barcelona Samuel Eto‘o amekosoa tasnia ya soka kwa kupoteza fedha nyingi kutokana na ukosefu wa uwekezaji. Anasema kwamba uhamisho wa kwanza wa mchezaji kati ya Afrika na Ulaya kwa kawaida hugharimu kati ya euro milioni 1 hadi 2, lakini mchezaji huyo huyo miezi sita baadaye anauzwa kwa euro milioni 30 hadi 40. Eto'o amesisitiza kuwa maendeleo ya soka ya Afrika sio sehemu ya maslahi ya Wazungu. "Sisi tulioishi Ulaya tumeona namna hii ya kutengeneza pesa, na tunataka wale wanaotuzunguka na wanaowekeza kwenye soka wapate pesa. Soka ni suala la kutafuta pesa. Lazima uwekeze, uwe na mpango wa kufanikisha hilo, na uyafanyie kazi mapato hayo," Eto'o alisema katika mahojiano na televisheni ya France 24.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement