Rais wa Klabu ya yanga Eng: Hersi Said amesifu ubora wa wachezaji wa Klabu ya Azam waliouonyesha katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara uliopigwa June 02 mwaka huu Uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar.

Eng: Hersi ameeleza kuwa Fainali hiyo ilikuwa yenye ubora sana kuliko Fainali za misimu iliyopita kutokana na ubora wa timu zote mbili sambamba na uwezo wa Mlinda mlango wa Azam FC Mohamed Mustapha.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza Azam FC wamecheza vizuri, sisi tulikuwa bora kuliko wao kwenye kila eneo lakini wao wameweza kucheza vizuri na kuifanya Fainali kuwa na thamani, lakini pia nimpongeze golikipa wao ameokoa nafasi nyingi na tungeweza kuzitumia labda tusingeweza kufika kwenye dakika za nyingeza n ahata hatua ya penati lakini haikuwa bahati yetu kumaliza mchezo mapema, ” Amesema Eng: Hersi Said – Rais wa Yanga SC.

Eng: Hersi amesema Michuano ya FA Cup ilikuwa ni michuano muhimu kwao na kuendelea kumiliki makombe ambayo walishachukua Back to Back.

Eng: Hersi pia ameweka wazi kuwa kufika hatua ya matuta haikuwa lengo lao kwani imekuwa na historia mbaya kutokana na kushindwa mashindano mawili kati ya matatu katika hatua ya matuta ikiwemo Fainali ya Ngao ya Jamii.

“Hatua ya penati kwangu mimi ilikuwa ya wasiwasi kwasababu tumecheza mashindano matatu mwaka huu na mawii tukashindwa kwa hatua ya matuta, kama mnakumbuka ngao ya jamii sisi tulitolewa kwenye hatua ya matuta na Ligi ya Mabingwa Afrika pia tulitolewa kwenye hatua ya matuta kwahiyo kwangu mimi hatua ya matuta haikuwa changuo na haikuwa kitu ambacho ningependa kitokee kwahiyo tunashukuru Mungu tumeweza kubadilisha matokeo, ” Amesema Eng: Hersi Said – Rais wa Yanga SC.

Eng: Hersi ameongeza kuwa mara baada ya kumaliza mchezo wa mwisho mwa msimu kwa sasa wanajipanga kwaajili ya msimu ujao kubwa ikiwa ni maandalizi pamoja na usajili kwa lengo kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa sambamba na kupambania Ngao ya Jamii ambayo waliipoteza msimu huu, kuteteta Ubingwa wa Ligi pamoja na FA.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement