Mchezaji huyo wa Napoli mwenye umri wa miaka 24 alinyakua tuzo katika tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) Jumatatu usiku, akishindana na nahodha wa Misri, Mohamed Salah na mlinzi wa Morocco Achraf Hakimi.

Kwa Osimhen, ambaye alikulia kwenye mitaa yenye vumbi ya Olusosun huko Lagos, ni "ndoto iliyotimia" baada ya kukabili hali halisi ya maisha akiwa mtoto.

"Lazima nimshukuru kila mtu ambaye amenisaidia katika safari hii na Waafrika wote ambao wamesaidia kuniweka kwenye ramani licha ya kasoro," Osimhen alisema.

Akilakiwa kila siku na uvundo kutoka kwa jalala katika mtaa wake, Osimhen anasema alikuwa na hamu kubwa ya kufanikiwa na alifanya kila awezalo kuwania ndoto hiyo, Ililazimika kuuza magazeti na maji ya chupa akielezea hali yake kuwa ya uchochole'

"Kama mvulana mdogo ambaye ilibidi atembee kwenye misongamano ya magari karibu kila siku ili kustahimili changamoto nyingi ambazo mimi na familia yangu tulikuwa tunakabiliana nazo, kuwa nyota mwenye thamani barani Afrika na katika kandanda ya ulimwengu ilikuwa ndoto isiyowezekana," alisema katika ujumbe uliotumwa kwenye X. "Safari yangu ya soka imekuwa ya panda shuka nyingi, Mabao na shangwe za ushindi hunifanya niendelee hata wakati ukosoaji, chuki na maumivu ya kushindwa yanaponipiga sana kifuani."

Baada ya kufunga mabao 26 na kuisaidia Napoli kutwaa taji la kwanza la ligi ya Italia katika kipindi cha miaka 33, Osimhen amekuwa Mnigeria wa kwanza kushinda tuzo ya Caf ya wanaume tangu mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nwankwo Kanu mwaka 1999.

"Alichofanya Osimhen ni cha ajabu," mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor, ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka wa 2008, aliiambia Caf TV.

"Kufunga mabao kunaweza kuwa rahisi Uingereza lakini kufanya hivyo nchini Italia sio rahisi kwa sababu wana ulinzi mkali na mbinu zenye hodari'.

Huku mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba, ambaye pia ni Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Caf mara mbili, akimtaja mshambuliaji huyo wa zamani wa Lille kama nyota mpya na mfalme mpya katika kandanda barani Afrika, sasa kuna matumaini kwamba anaweza kuisaidia Nigeria kuelekea kwenye enzi mpya ya mafanikio.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement