Mfungaji bora wa Michuano ya AFCON Emilio Nsue ambaye alitangaza kustaafu baada ya kutofautiana na Shirikisho la soka la nchi yake, amekubali kurejea kuisaidia Equatorial Guinea katika kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Emilio Nsue anarejea baada ya vikao mfululizo vilivyofanywa ili kumshawishi kurejea ndani ya timu ya taifa na sasa anaonekana yupo tayari.

Nsue atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaojumuishwa kikosini katika mechi zijazo mwezi Juni.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement