Ekitike, mwenye umri wa miaka 23, alifunga bao la ushindi dakika ya 85, lakini akaonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kuvua jezi wakati akisherehekea. Hatua hiyo ilimfanya referee Thomas Bramall kumtuma nje dakika chache baada ya mashangilio kumalizika.

Kwa mujibu wa kanuni, mshambuliaji huyo sasa atakosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki, hali ambayo imemuweka kocha Arne Slot kwenye wakati mgumu wa kupanga kikosi.

Kupitia Instagram Story yake, Ekitike aliandika:

“Nilifurahi sana kuisaidia timu kupata ushindi katika mechi yangu ya kwanza ya Carabao Cup hapa nyumbani. Lakini hisia zilinizidi. Samahani kwa familia ya Reds. Nashukuru kwa mashabiki kwa msaada wao na wachezaji wenzangu kwa kufanikisha ushindi huu.”


Baada ya mchezo, kocha Slot hakuficha hasira zake kwa kitendo hicho, akieleza kwamba Ekitike alipaswa kujizuia.

“Kadi ya kwanza ilikuwa ya kipuuzi kwa sababu unapaswa kudhibiti hisia zako. Nafahamu ugumu wa kucheza namba tisa katika Premier League, lakini bado unahitaji busara. Ukishindwa kujizuia, basi usifanye jambo linalokupeleka kwenye kadi. Kwa hiyo, ndiyo, ilikuwa si jambo la busara — unaweza kuita ni kijinga.”

Slot aliongeza kwamba aina ya sherehe iliyompelekea Ekitike kutolewa nje ingeweza kueleweka endapo ingekuwa mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa, lakini si kwa mchezo wa Kombe la Ligi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement