Droo ya Michuano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika inatarajiwa kufanyika Julai 11 mwaka huu 2024 Cairo nchini Misri.

Wawakilishi wa Tanzania kunako Michuano hiyo kwa maana ya Yanga SC, Azam FC, Coastal Union na Simba SC watawajua wapinzani wao watakaokutana nao katika Mashindano mawili Makubwa Barani Afrika.

Yanga SC na Azam FC ndio Wawakilishi wa Tanzania Klabu bingwa barani Afrika huku Simba SC na Coastal Union ya Tanga zikiwa zimeangukia kunako mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Kwa upande wa Burundi, Vital’O FC ndio watakao iwakilisha nchi hiyo kwenye Klabu Bingwa huku Rukinzo FC timu ya Polisi wao wakiwa katika Mashindano ya Shirikisho.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement