Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)hii leo litaendesha Droo ya Hatua za awali za Msimu wa CAF 2024/25 Interclub kwenye Makao Makuu ya CAF Cairo, Misri.

Droo ya Hatua ya Awali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF ya Ligi ya Mabingwa sambamba na Shirikisho Afrika inaashiria kuanza rasmi kwa kile kinachoahidi kuwa msimu mwingine soka la klabu bora Afrika.

Kwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni jumla ya klabu 59 zitashiriki kutoka nchi 47 za Afrika, huku Kombe la Shirikisho litakuwa na klabu 52 zinazowakilisha nchi 41.

Mashindano ya CAF Interclub ya wanaume yamesalia kuwa mashindano mawili ya klabu yanayotafutwa sana katika soka ya vilabu barani Afrika, huku mashindano yote mawili yakiendelea kukua kutoka nguvu hadi nguvu, yakifurahia rekodi ya watazamaji wa televisheni duniani kutokana na kiwango kinachoongezeka cha soka barani Afrika.

Ni wawakilishi wa Tanzania, Yanga SC na Azam Fc ambao watashiriki ligi ya mabingwa wakati Simba na Coastal Union watashiriki kombe la Shirikisho

Katika msimu uliopita, mabingwa watetezi Al Ahly SC waliongeza mataji yao ya Ligi ya Mabingwa hadi hadi kufikia idadi ya makombe 12, huku wapinzani wao Zamalek wakitawazwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF kwa mara ya pili.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement