Kwa mara ya kwanza Tanzania na Afrika mashariki zinajivunia kuwa na timu 2 kwenye robo finali za Kombe la Klabu bingwa Afrika (CAF Champions League) kufuatia ufanisi murua wa Simba na Yanga.

Simba na Yanga, pia ndio timu pekee kutoka eneo moja hususan Afrika mashariki na pia kuwa ndio timu zilizofunga magoli mengi hatua ya makundi, (magoli 9).

Je ni kina nani wanawasubiri Simba na Yanga hatua ya robo fainali kwenye droo itakayojulikana tarehe 5 Machi.

Miamba hao wa bongo wanaweza kukutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly ya Misri na Petro de Luanda ya Angola na Asec ya Ivory Coast.

Simba na Yanga zitaanzia michuano ya robo fainali nyumbani Machi 29 - 31 na kumalizia mkondo wa pili ugenini.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement