DKT KAILIMA ATEULIWA KUWA MJUMBE BODI YA WAKURUGENZI SIMBA SPORTS CLUB
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu amemteua, Dr. Kailima Ramadhani Kombwey kuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company Limited.
Taarifa ya Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo imebainisha kuwa Dkt. Kailima ataungana na wajumbe wengine waliochaguliwa kuiwakilisha Simba Sports Club katika bodi ya Wakurugenzi, sambamba na wajumbe wengine walioteuliwa na Muwekezaji, Mohammed Dewji.
“Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 27 (1) (d) ya Katiba ya Simba Sports Club, 2018 (Kama ilivyofanyiwa mare kebisho 2024) inayompa mamlaka Mwenyekiti wa Klabu kuteua wajumbe wawili wa bodi. Uteuzi huu unaanza kazi mara moja.” --- imesema taarifa hiyo.