BAADA ya maswali mengi kuhusu kuachwa kwa mastaa sita wa kikosi cha kwanza cha Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ametoa sababu za kuachwa nyota hao.

Wachezaji walioachwa kwenye msafara wa Yanga ambayo inacheza na Namungo jioni ya leo ni Djigui Diarra, Joyce Lomalisa, Khalid Aucho, Keneddy Musonda, Pacome Zouzoua na Joseph Guede.

Gamondi amesema anatambua umuhimu wa wachezaji hao kikosini kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwenye michezo iliyopita, lakini ameamua kuwapa muda wa kujitibia majeraha madogo madogo waliyoyapata na wengine kumaliza matatizo waliyonayo.

"Kwa asilimia kubwa ni wachezaji muhimu kikosini, lakini wana shida ambazo tungeziweka pembeni ingeleta shida kwani wasingecheza kwa ubora tunaoufahamu kutoka kwao," amesema.

"Sipendi kuweka wazi shida ya kila mmoja inatakiwa kueleweka kuwa kuna ambao wana maje-raha madodomadogo na wengine shida za kifamilia."

Pia, Gamondi amesema itachangia kuwapa muda wa kuwa fiti zaidi kwa mechi nyingine zilizo mbele yao huku akiitaja Ihefu FC na Geita Gold michezo ambayo watacheza uwanja wa nyumbani.

"Baada ya mechi ya leo na Namungo tutakuwa na siku mbili tu tayari kwa mchezo mwingine wa ligi, hivyo kutoa nafasi za baadhi ya wachezaji ambao hawapo fiti kutokana na majeraha madogo madogo itatusaidia," amesema kocha huyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement