dereva wa kampuni ya Ferrari Charles Leclerc amesema amejipanga kuhakikisha anashinda tena kwenye mbio zijazo kwenye mashindano ambayo yatafanyika huko Canada siku ya Jumapili tarehe 9 ya mwezi juni 

Leclerc ni dereva mkongwe kwenye kampuni ya Ferrari lakini kwa msimu huu ameshinda mara moja kwenye grand prix ambayo imefanyika huko Monaco May 26 ,mipango ya leclerc ni kushinda ubingwa wa Champioship ubingwa ambao umechukuliwa mara tatu mfululizo na kampuni ya Red bull kupitia dereva wake Max Varstapen.

kwa msimu ujao kampuni ya Ferrari itakuwa na dereva mkongwe Lewis Himilton ambaye amepata mafanikio makubwa na kampuni ya Mercedes ambayo imempa nafasi ya kushinda ubingwa wa champioship mara saba sambasamba na dereva mkongwe raia wa ujerumani Michael Schumarcher.

Lewis Himilton atajiunga na Ferrari kuchukua nafasi ya dereva Carlos Saiz ambaye pia anahusishwa kujiunga na Mclaren mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizka 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement