BARCELONA, HISPANIA, Taarifa za siri kutoka kwenye mahakama inayoendesha kesi ya ubakaji inayomuhusu Dani Alves, zimefichua beki huyo wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil huenda akatupwa jela miaka nane.

Taarifa hizo zinasema, waendesha mashtaka wa kesi hiyo, inadaiwa watamshtaki Alves kutokana na kesi ya ubakaji inayomkabili na atatakiwa kumlipa mwathirika wa tukio hilo, Pauni 130,000, Beki huyo mwenye umri wa miaka 40 bado yupo rumande wakati kesi yake ikendelea kurindima, bila ya kuwekewa dhamana tangu mwezi Januari mwaka huu.

Madai dhidi yake yalikuwa kama "unyanyasaji wa kijinsia" hadi hati ya mashtaka ilipotolewa Hispania tangu mwaka jana. Lakini Alves alipinga shutuma hizo akidai walikubaliana na mwanamke huyo kufanya tendo la ndoa nje ya baa iliyopo Barcelona. Alvez alimwomba radhi mkewe Joana Sanz ambaye ni mwanamitindo maarufu kutoka Brazil, hata hivyo ndoa yao imevunjika rasmi.

Katika mahojiano aliyofanyiwa akiwa rumande, Alves alisema: "Mtu pekee ninayepaswa kumwomba msamaha ni mke wangu, Joana Sanz. Tayari nimemwomba radhi alipokuja hapa gerezani kuniona, lakini lazima nimwombe tena hadharani kila mtu ashuhudie. Kwa sababu kesi yangu ipo hadharani kila mtu anafahamu, anastahili kupewa msahama bila kuficha." Desemba mwaka jana Qatar, Alves alikua mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuiwakilisha Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement