Nyota wa soka raia wa Brazil, Dani Alves anaweza kuachiwa huru kwa masharti ya kulipa dhamana ya Euro Milioni 1 (Tsh. Bilioni 2.8) baada ya kutumikia takriban robo ya kifungo chake cha miaka minne na nusu kilichotokana na madai ya ubakaji

Beki huyo wa zamani wa FC Barcelona, Juventus na Timu ya Taifa ya Brazil amekata rufaa na kuomba awe nje wakati rufaa yake ikisikilizwa, amekubaliwa lakini kwa masharti ya kushikiliwa kwa Pasi zake za Kusafiria za Brazil na Uhispania, pia awe anafika mbele ya Mahakama kila wiki. 

Aidha, Mahakama ilitoa amri ya kumzuia Alves kumkaribia mwathiriwa. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement