DANI ALVES AHUKUMIWA JELA MIAKA MINNE
Mahakama ya Juu ya Catalonia Nchini Hispania imemuhukumu kwenda jela miaka minne na nusu Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil na Club ya Barcelona Dani Alves (40) baada ya kukutwa na hatia ya kosa la shambulio la ngono au unyanyasaji wa kingono kwa Mwanamke mmoja kwenye Club ya usiku.
Pamoja na hukumu hiyo, Alves ambaye amekua rumande tangu mwaka 2023 akisubiri hukumu hii, ametakiwa kumlipa fidia ya euro 150,000 (Tsh milioni 414) Mwanamke huyo.