DAKIKA 90 ZA SIMBA NA GALAXY HAZITAKUWA RAHISI
Mohammed Hussein Tshabalala' amesema dakika 90 za mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaopigwa leo ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy hazitakuwa rahisi lakini wamejiandaa kushindana ili kupata pointi tatu muhimu na wanakumbuka vizuri sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Tshabalala alisema licha ya ubora wa Jwaneng, lakini wamepania jambo moja tu, kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao wa pili hatua ya makundi ili kuwarudisha mashabiki na siosi wenyewe kwenye ushindani. "Tunajua haitakuwa rahisi, tunakutana na timu nzuri hatuwezi kuweka malengo yetu pembeni kwa kuhofia ubora wa wapinzani tunapambana kuhakikisha tunaendeleza rekodi yetu nzuri ya kutinga hatua na nusu fainali na hatimaye kucheza fainali," alisema beki huyo wa kushoto na kuongeza;
"Imani yangu kubwa inatokana na namna ambavyo uongozi, benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla kuumizwa na matokeo mabaya tuliyoyapata kwwenye mechi tatu mfululizo tukikubali kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa mtani, sare ya 1-1 na Namungo na kuanza vibaya mchezo wa kwanza wa makundi" Tshabalala alisema motisha waliyopewa na viongozi, wanachama na benchi la ufundi wakiwasisitiza kuwa wanatakiwa kupambana na bado wanafasi ya kufanya vizuri imewapa nguvu na watapambana kutoa jasho ndani ya dakika 90 ili kuwapa furaha mashabiki zao ambayo wameikosa kwa muda.
"Tunapitia nyakati ngumu ambayo haijazoeleka na mashabiki tunaelewa ugumu wanaoupata sisi pia tunaumizwa na matokeo tumewasikia natutafanyia kazi kwenye mchezo kwa kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kurudi kwenye ushindani tuliouzoea" alisema mchezaji huyo mwandamizi kwa sasa katika kikosi hicho cha Simba ambaye aliongeza;
"Akili yetu sasa ipo kwa Jwaneng ni mechi ngumu kwetu na tutaingia kwa kuwaheshimu wapinzani wetu lengo ni kuona namna ambavyo tutawakabiri wapinzani wetu kuhusu kuchelewa kuondoka ni mipango ya benchi la ufundi na haliingiliani na mchezo kwani tunafika siku moja kabla hivyo kuwahi au kuchelewa ni mambo mawili tofauti kwenye dakika 90 za mchezo."