Mara baada ya mchezo wa kirafiki kukamilika baina ya taifa la Ureno dhidi ya taifa la Ireland na kushuhudia Ureno akishinda mabao 3 kwa sifuri basii mchezo huo umepelekea Ronaldo kuweka REKODI nyingne 

Cr7 aliweza kufunga mabao 2 katika Ushindi huo na kupelekea kufikisha idadi ya mabao 130 katika michezo 207 aliyo tumikia taifa hilo la ureno akiwa kijana mpaka sasa

Baada ya mchezo huo ameweza kuzungumza na kusema kua siku zote mpira ndio kitu anacho kipenda ndio maana anajituma na hata anavyo cheza nikama vile vile akiwa na umri wa miaka 20 na akidai kua na michuano hii ya uefa euro atakipiga kwa kiwango kile kile

Kumbuka mchezo wa kwanza utakua ni siku ya jumanne dhidi ya jamuhuri ya cech, hivyo tunatarajia kuona ubora ule ule wa Ronaldo

Pia Ronaldo amefikisha mabao 895 kiujumla tangu alivyo anza kucheza kandanda mpaka leo hii akiwa na umri wa miaka 39 hivyo anahitaji MABAO 5 kuweka REKODI mpya ya mabao 900 na kua mchezaji wa kwanza kufanikwa kufikisha mabao hayo akiwa na umri wa miaka 39

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement