COPA AMERICA KUJA NA KADI YA PINK YA UWAMUZI WA MAJERAHA YA UWANJANI
Kuelekea mashindano ya copa america ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi wa sita kumeibuka mjadala mpya baada ya kueleza kua kadi yenye rangi ya pinki itatambilishwa na kuungana na kadi ya njano na nyekundu kama sehemu ya mchzo na zote tutarajie zikitumika kwa kazi tofuati japo tunajua kua kadi ya njano na nyekundu zipo muda mrefu ila stori kubwa ni hii KADI ya pink.
Kadi hii ya pink inaazashishwa kama sheria mpya kwa lengo la kulinda afya za wachezaji, Mchezo ukiwa unaendelea itatokea mchezaji kapata jeraha la kichwa ambalo hawezi kumudu kucheza mchezo basi Kocha atamfata mwamuzi wa akiba (Fourth official) nae mwamuzi huyoo ataweza kumpa taarifa mwamuzi wa kati (refa) na hapo itanyanyuliwa juu kadi ya Pink.
Sasa kadi hiyo ya Pink ikioneshwa juu mchezaji huyu atatolewa nje moja kwa moja kwenda kupata matibabu na hata rejea tena uwanjani kuendelea na Mchezo kwa maana kadi hiyo ya Pink ni kulinda afya ya mchezaji husika.
Lakini pia kuanzishwa kwa kadi hii ya Pink kutapelekea pia mabadiriko ya wachezaji kutoka wa 5 hadii 6 kwa sababu mchezaji huyu ambae ataoneshwa kadi ya pink hata rudi uwanjani hivyo ndo maana wameona waongeze idadi ya mchezaji mmoja wa akiba na kufanya wawe 6.
Hata hivyo bado haijathibitishwa rasmi maana mapendekezo haya yameanza tarehe 23 siku ya j5 mwaka 2024 na inaonekanaa kuna uwezekano mkubwaa kadi ya pink tukaishuhudia copa america na duniani kote