CLATOUS CHAMA, KIBU DENIS, MIQUISSONE KUONGOZA MASHAMBULIZI DHIDI YA ASEC MIMOSAS
KIKOSI cha Simba kimeondoka nchini leo alfajiri kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Ijumaa hii ya Februari 24 huku ikimkosa kipa, Ayoub Lakred kutokana na kupata kadi tatu za njano na mshambuliaji, Leandre Onana kwa sababu ya majeraha
Lakred atashindwa kucheza mchezo huo kutokana na kanuni zinazomzuia baada ya kupata kadi hizo wakati wa mchezo baina ya timu hiyo dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kisha mechi mbili mfululizo na Wydad Casablanca kutoka nchi ya Morocco.
Kumkosa Lakred sio pigo zaidi kwa Simba kutokana na uwepo wa kipa, Aishi Manula ambaye amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi hicho licha ya hivi michezo ya hivi karibuni tangu aliporudi akitokea majeruhi kubadilishana na makipa wengine.
Eneo la ushambuliaji watakuwepo mastaa wapya wa timu hiyo Pa Omary Jobe na Freddy Michael.
Simba iliyokuwa kundi 'B' na pointi tano inahitaji kushinda zaidi mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali tofauti na wapinzani wao ASEC Mimosas ambayo tayari imeshafuzu baada ya kufikisha pointi 10.